Mbowe, viongozi wenzake waachiwa kwa dhamana

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imewaachia kwa dhamana Mwenyekiti wa Taifa wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe na viongozi wenzake baada ya kutimiza masharti ya dhamana leo Aprili 3, 2018.
Masharti hayo ni kusaini bondi ya Shilingi milioni 20, kuwa na wadhamini wawili wenye barua kutoka ofisi za Serikali za mitaa au vijiji na kuripoti kituo kikuu cha Polisi kila Alhamisi.
Mbowe na wenzake wamefikishwa mahakamani leo asubuhi saa mbili ili wakamilishe masharti ya dhamana.
Mbali ya Mbowe wengine ni Katibu Mkuu Dk Vicent Mashinji, Manaibu Katibu wakuu John Mnyika (Bara), Salum Mwalimu (Zanzibar), Mbunge wa Iringa mjini Mchungaji Peter Msigwa na Mweka Hazina wa Baraza la Wanawake wa chama hicho Ester Matiku wanakabiliwa na kesi ya jinai, wakidaiwa pamoja na mambo mengine ikiwamo kufanya mikusanyiko na maandamano yasiyo halali.
Wamekuwa mahabusu tangu walipopandishwa kizimbani na kusomewa mashtaka hayo Machi 27, 2018.
Share on Google Plus
Ahsante kwa kutembelea site yangu, unaweza kunicheki kwenye mitandao ya kijamii kwa kubonyeza icons juu kulia na kunipata moja kwa moja kwenye Facebook, Twitter na Instagram...Endelea kuwa karibu yangu ili uweze kufikiwa na chochote kinachonifika.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 Maoni:

Post a Comment