Naibu
Spika, Tulia Ackson, leo Aprili 3 amewaapisha wabunge wawili, Dk Godwin Mollel
wa jimbo la Siha na Maulid Mtulia wa jimbo la
Kinondoni.
Wabunge
hao wameapishwa baada ya kufanyika kwa uchaguzi mdogo katika majimbo ya Siha na
Kinondoni, baada ya wabunge wa maeneo hayo kuhamia CCM.
Mtulia,
alikuwa mbunge wa Kinondoni (CUF), kabla ya kuhamia CCM na kugombea tena jimbo
hilo kwa kupitia CCM.
Kadhalika
Mollel, alikuwa mbunge wa Siha, (Chadema) kabla ya kuhamia CCM na kugombea tena
jimbo hilo kwa tiketi ya CCM.
Hata
hivyo kiapo hicho hakikushuhudiwa na idadi kubwa ya wabunge wa upinzani ambao
hawakuwepo katika kikao cha leo.
Hili
ni bunge la kumi na moja na mkutano wa kumi na moja.
M
0 Maoni:
Post a Comment