Serikali kutaifisha mashamba ya watu wanaolima dawa za kulevya

Waziri wa Mambo ya Ndani, Mwigulu Nchemba, amesema serikali imeanza kuainisha mashamba ya watu wanaojihusisha na kilimo cha dawa za kulevya aina ya mirungi katika Wilaya ya Same mkoani Kilimanjaro, ili kuyataifisha.
Ameyasema hayo, kwenye harambee ya kuchangia ujenzi wa kanisa la Kiinjli la Kilutheri Tanzania (KKKT) Dayosisi ya Pare Usharika wa Masaka, wilayani humo.
Amesema kuwa serikali imeanza kuainisha mashamba hayo ya watu binafsi ambao wamekaidi agizo la serikali na kuendeleza kilimo cha dawa za kulevya kinyume cha sheria.
“Tukishamaliza kuyaainisha mashamba yote yanayolima dawa za kulevya, serikali itayataifisha na wamiliki kufungwa jela miaka 30. Same ni miongoni mwa wilaya zinazoongoza kwa kilimo cha mirungi, nawashauri ni vema mkaachana na biashara hiyo na kujihusisha na kilimo cha mazao mengine ya biashara na chakula,” amesema Mwigulu.
Share on Google Plus
Ahsante kwa kutembelea site yangu, unaweza kunicheki kwenye mitandao ya kijamii kwa kubonyeza icons juu kulia na kunipata moja kwa moja kwenye Facebook, Twitter na Instagram...Endelea kuwa karibu yangu ili uweze kufikiwa na chochote kinachonifika.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 Maoni:

Post a Comment