BREAKING NEWS: MAHAKAMA YAWAACHIA KWA DHAMANA YA SH MIL 20 KILA MMOJA VIONGOZI 6 WA CHADEMA


Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imetoa masharti ya dhamana kwa viongozi 6 wa CHADEMA akiwemo Freeman Mbowe kwa kuwa na wadhamini 2 kila mshtakiwa atakayesaini Bondi ya Shilingi Milioni 20.

Pia wadhamini hao wawe na barua za utambulisho, ambapo baada ya kutimizwa masharti hayo Mbowe na wenzake wawe wanaripoti Central Police mara moja kwa wiki.

Wakili wa serikali, Faraja Nchimbi ameieleza Mahakama ya Kisutu kuwa watakata rufaa kupinga uamuzi wa mahakama hiyo kutoa masharti ya dhamana kwa Mbowe na wenzake
Share on Google Plus
Ahsante kwa kutembelea site yangu, unaweza kunicheki kwenye mitandao ya kijamii kwa kubonyeza icons juu kulia na kunipata moja kwa moja kwenye Facebook, Twitter na Instagram...Endelea kuwa karibu yangu ili uweze kufikiwa na chochote kinachonifika.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 Maoni:

Post a Comment