Mwanafunzi
wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Kumbusho Dawson anashikiliwa na
polisi akituhumiwa kusambaza picha kuonyesha nyufa kwenye majengo ya
hosteli.
Ahsante kwa kutembelea site yangu, unaweza kunicheki kwenye mitandao ya kijamii kwa kubonyeza icons juu kulia na kunipata moja kwa moja kwenye Facebook, Twitter na Instagram...Endelea kuwa karibu yangu ili uweze kufikiwa na chochote kinachonifika.
Dawson ambaye ni mbunge wa serikali ya wanafunzi (Daruso) alikamatwa jana Jumatatu Desemba 4,2017 mchana.
Makamu wa Rais wa Daruso, Anastazia Anthony amethibitisha kukamatwa kwa mbunge huyo jana saa saba mchana.
"Ni
kweli Kumbusho alikamatwa jana mchana na kupelekwa kituo cha polisi
cha Chuo Kikuu kwa ajili ya kuhojiwa lakini ilipofika saa tisa alasiri
polisi walisema hawana uwezo wa kumuhoji hapa hivyo wakampeleka
Oysterbay," amesema Anastazia.
Kamanda
wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa alipotafutwa
amesema hana taarifa kuhusu tukio hilo. Alisema anasubiri
atakapofikishiwa taarifa atazitoa kwa umma.
0 Maoni:
Post a Comment