ASKARI WATAKIWA KUFANYA MAZOEZI

Kamanda wa Kanda Maalum ya Kipolisi ya Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa
KAMANDA wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa amewataka askari kufanya mazoezi ya viungo ili kujiweka imara sambamba na kujenga afya zao.
Kamanda Mambosasa aliyasema hayo jana jijini Dar es Salaam, wakati aliposhiriki katika matembezi na mazoezi ya viungo na askari wa vikosi vya Kanda Maalumu ya Dar es Salaam. Alisema askari na jamii kwa ujumla wanapaswa kufanya mazoezi pale wanapopata nafasi na siyo mpaka walazimishwe, kwani mazoezi yanasaidia kujenga mwili na kuepusha mwili na magonjwa yasiyoambukiza kama kisukari na shinikizo la damu.
“Mazoezi haya yanatakiwa kuwa endelevu kwa askari wote wa polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, mazoezi haya yanajenga urafiki na kuimarisha ujirani mwema na pia yanaweka mwili imara,” alisema. Matembezi hayo ya ‘Root Match’ yalifanyika katika mikoa ya kipolisi Temeke na Kinondoni na yatakuwa yakifanyika kila Jumamosi ya mwisho wa mwezi
Share on Google Plus
Ahsante kwa kutembelea site yangu, unaweza kunicheki kwenye mitandao ya kijamii kwa kubonyeza icons juu kulia na kunipata moja kwa moja kwenye Facebook, Twitter na Instagram...Endelea kuwa karibu yangu ili uweze kufikiwa na chochote kinachonifika.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 Maoni:

Post a Comment