Hii ndio sababu ya kulazwa rumande kwa mnunuzi nyumba za Lugumi


Dar es Salaam. Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam linamtuhumu Dk Louis Shika kutumwa na mfanyabiashara, Said Lugumi, kukwamisha mchakato wa kuziuza nyumba zake kwa mnada.
Akizungumza na Mwananchi leo (Ijumaa), Novemba 10, Kamanda wa Kanda hiyo, Lazaro Mambosasa amesema mazingira ya mnada na jinsi alivyokuwa akifika bei ya kununua nyumba hizo yamelifanya jeshi hilo lihisi ametumwa kukwamisha uuzaji huo.

“Aliwekwa na Lugumi mwenyewe ili mnada usifanyie ingawa sina fact (vielelezo) za kudhibitisha hilo, ila alichokuwa anakifanya kinatufanya tuamini hivyo. Alikuwa ana top (anapandisha) bei kila nyumba ili washiriki wengine wasinunue,

Ila jinsi alivyo, kwa maana ya uvaaji na kuongea kwake watu walitia mashaka kama ataweza kununua ndipo akatakiwa kutoa asilimia 25 na kushindwa kulipa. Tunaendelea kumshikilia kwa mahojiano,” amesema  Mambosasa

Mwananchi lilipotaka kujua iwapo mtuhumiwa huyo amemtaja Lugumi katika mahojiano ya awali, Kamanda Mambosasa amesema upelelezi unaendelea na umma utapewa taarifa utakapokamilika.

Source: Mwananchi
Share on Google Plus
Ahsante kwa kutembelea site yangu, unaweza kunicheki kwenye mitandao ya kijamii kwa kubonyeza icons juu kulia na kunipata moja kwa moja kwenye Facebook, Twitter na Instagram...Endelea kuwa karibu yangu ili uweze kufikiwa na chochote kinachonifika.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 Maoni:

Post a Comment