Msondo
Ngoma kupitia kampuni ya Mawakili ya Maxim imeitaka Wasafi Clasic Baby
(WCB) kuwalipa fidia ya kiasi cha shilingi 300 milioni kutokana na
kutumia kionjo hicho cha muziki kilichotungwa na kupigwa katika wimbo
wao wa ‘Ajali’ na kukirudia katika wimbo wao wa ‘Zilipendwa’ bila kupata
idhini ya mmiliki.
Kionjo
hicho kilichotungwa na kupigwa kuanzia dakika ya 6:38 hadi 6:52 kwenye
wimbo wa ‘Ajali’ mali ya Msondo Ngoma, kimeigwa na kupigwa katika wimbo
wa ‘Zilipendwa’ kuanzia dakika ya 4:55 hadi 5:10.
Barua
hiyo imeitaka WCB kulipa fedha hizo ndani ya muda wa siku saba na kama
wakishindwa basi Msondo Ngoma watawachukulia hatua zaidi za kisheria.


0 Maoni:
Post a Comment