WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa amewataka wanafunzi wa kike wanaosoma katika shule mbalimbali nchini kusoma kwa bidii na wasikubali kushawishika.
Ahsante kwa kutembelea site yangu, unaweza kunicheki kwenye mitandao ya kijamii kwa kubonyeza icons juu kulia na kunipata moja kwa moja kwenye Facebook, Twitter na Instagram...Endelea kuwa karibu yangu ili uweze kufikiwa na chochote kinachonifika.
Pia Waziri Mkuu amesema serikali imeweka sheria kali kwa wote watakaobainika kukatisha masomo ya watoto wa kike kwa kuwapa ujauzito au kuwaozesha. Waziri Mkuu alitoa kauli hiyo juzi wakati akizungumza na wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Wasichana na WAMA Sharaf.
Shule ambayo ipo wilayani Lindi inamilikiwa na Taasisi ya WAMA, ambayo inasomesha watoto wa kike ambao ni yatima na wanaotoka katika mazingira magumu. Waziri Mkuu aliwataka wanafunzi hao wa kike kuhakikisha wanatumia muda wao vizuri kwa kusoma kwa bidii na hatimaye watimize malengo yao.
Naye Mwenyekiti wa Taasisi ya Wama, Mama Salma Kikwete ambaye pia ni Mbunge wa Kuteuliwa, alisema shule hiyo inasomesha watoto yatima na wanaoishi katika mazingira magumu kutoka mikoa yote nchini.
0 Maoni:
Post a Comment