Wasabato wamuunga mkono JPM 100%


KANISA la Waadventista Wasabato, Jimbo la Kusini Mashariki mwa Tanzania (SEC), limesema linaunga mkono kwa asilimia 100 jitihada za Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Rais John Magufuli katika jitihada zake za maendeleo, ikiwemo kupiga vita na kutokomeza dawa za kulevya nchini.

Askofu na Mwenyekiti wa Jimbo la Kusini Mashariki mwa Tanzania (SEC), Mchungaji Herbert Nziku, alisema kanisa hilo linaunga mkono serikali kwa vitendo ambapo linaendesha kampeni ya kupinga usafirishaji, biashara na matumizi ya dawa za kulevya. “Tatizo la dawa za kulevya limetokea kuwa janga kubwa duniani kote, watu wengi wameathirika na janga hili...Tusipokubali kufanya uamuzi wa busara katika kuunga mkono juhudi za serikali yetu za kupambana na biashara na matumizi ya dawa hizi, kuna hatari kwa jamii yetu na Taifa letu la Tanzania kugeuka kuwa jalala na wodi za waathirika wa dawa za kulevya,” alisema.

Alisema: “Kanisa la Waadventista Wasabato linamtaka kila mtu na kila taifa kushiriki katika kutokomeza mlipuko wa biashara na matumizi ya dawa za kulevya ulioenea duniani kote, biashara ambayo inashusha hadhi ya jamii katika mataifa na kuwaangamiza walioathirika na kuwafanya waishi maisha ya uhalifu”.

Nziku alisema kanisa linatambua kuwa kufanya biashara, matumizi mabaya na kusafirisha dawa za
kulevya ni chukizo mbele za Mungu, ni hatari kwa afya za watumiaji, hukosesha furaha familia na jamii, hudhoofisha nguvu kazi ya taifa na kuzidisha umasikini katika taifa.

Alitoa mwito kwa wazazi, walezi na walimu kutoa elimu kwa watoto na vijana ili kuikinga jamii dhidi matumizi ya dawa hizo na kuiomba serikali kupitia wizara zinazohusika kuandaa mitaala ya somo hilo kuanzia shule za misingi hadi vyuo vikuu.
Share on Google Plus
Ahsante kwa kutembelea site yangu, unaweza kunicheki kwenye mitandao ya kijamii kwa kubonyeza icons juu kulia na kunipata moja kwa moja kwenye Facebook, Twitter na Instagram...Endelea kuwa karibu yangu ili uweze kufikiwa na chochote kinachonifika.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 Maoni:

Post a Comment