
Matumaini ya Muingereza Johanna
Konta kufika fainali za Wimbledon yamefutiliwa mbali baada ya kuchapwa
na Venus Williams wa Marekani katika hatua ya nusu fainali.
Konta anayeshikilia nafasi ya sita kwa ubora duniani, alitegemea kufika fainali hizo na kuwa wa kwanza kufanya hivyo kwa Uingereza tokea mwaka 1977.

Matumaini pekee kwa Konta ni kuingia ndani ya tano bora kwa ubora.
Venus atachuana na Garbine Muguruza wa Hispania aliyemchapa Magdalena Rybarikova wa Slovakia kwa seti 6-1 6-1.
0 Maoni:
Post a Comment