RPC aeleza utoro wa mtuhumiwa

http://www.habarileo.co.tz/images/HAMDUI.jpg
KAMANDA wa Polisi Mkoa wa Kipolisi Ilala, Salum Hamduni ameieleza Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kuwa mshitakiwa Hassan Nuru, anayekabiliwa na mashitaka ya wizi wa mafuta ya petroli na dizeli yenye thamani ya Sh milioni 239, kuwa aliwatoroka akiwa Kituo Kikuu cha Polisi Dar es Salaam.

Hamduni alitoa madai hayo jana mbele ya Hakimu Mkazi, Huruma Shaidi baada ya Wakili wa Serikali, Salum Msemo kudai kuwa kesi hiyo imekuja kwa ajili ya kusikilizwa. Alidai mshitakiwa huyo ambaye pia alijitambulisha kama Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Hashi Energy (T) Ltd alitakiwa kurejesha kielelezo ambacho ni malori matatu ya mafuta ili polisi waendelee na upelelezi.

Alidai, Januari 2015 akiwa Mkuu wa Upelelezi Mkoa wa Kipolisi Ilala, alipokea mafaili yenye makosa ya jinai likiwemo la wizi wa mali isafirishwayo kutoka kwa Kamishna Msaidizi wa Polisi, ACP David Mnyambugha. Akiongozwa na Wakili Msemo, Kamanda huyo alidai yalitoka maagizo kwamba kielelezo kilichopokelewa na Nuru kirudishwe Polisi ambayo ni malori matatu yenye mafuta ya petroli na dizeli na kwamba Februari 14, 2015 aliandika barua kwa Kampuni ya Hashi ili kurudisha vielelezo hivyo walivyopewa na Mkurugenzi wa Makosa ya Jinai.

Pia alidai, katika barua hiyo aliielekeza kampuni hiyo irudishe kielelezo hicho ifikapo Februari 16, 2015 ikiwa ni pamoja na kumpigia simu Nuru kwa kuwa yeye ndiye aliyekabidhiwa kielelezo hicho. Aliendelea kudai kuwa kilelezo hakijarudishwa na badala yake mshitakiwa alifika ofisini kwake na wakili wake ambapo aliwaelimisha kuwa kielelezo walipewa kwa ajili ya kutunza na kinapohitajika kinatakiwa kurudishwa. Alieleza wakati wanatoka ofisi ya Mkuu wa Upelelezi, kabla ya kuingia katika ofisi yake, walimuona mshitakiwa akiongea na simu na kwamba yeye na wakili wake wakaendelea na kuingia ofisi na walipotazama nyuma hawakumuona mshitakiwa huyo.

Share on Google Plus
Ahsante kwa kutembelea site yangu, unaweza kunicheki kwenye mitandao ya kijamii kwa kubonyeza icons juu kulia na kunipata moja kwa moja kwenye Facebook, Twitter na Instagram...Endelea kuwa karibu yangu ili uweze kufikiwa na chochote kinachonifika.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 Maoni:

Post a Comment