WINGA Deus Kaseke ameandikisha historia
nyingine kwenye maisha yake ya kucheza kandanda baada ya usiku wa
kuamkia leo kujiunga na timu iliyopanda daraja ya Singida United kwa
mkataba wa miaka miwili.
Kaseke anayecheza nafasi ya winga ya
kushoto amejiunga na Singida United inayonolewa na kocha wake wa zamani
Mdachi Hans Van Pluijm,akiwa mchezaji huru baada ya kumaliza mkataba
wake na mabingwa watetezi wa taji la ligi kuu bara,Yanga.
Kaseke alijiunga na Yanga miaka miwili iliyopita akitokea Mbeya City ya mkoani Mbeya kwa ada ya uhamisho ya Shilingi Milioni 35.
Akiwa na Yanga,Kaseke aliisaidia timu
hiyo ya mtaa wa Jangwani kutwaa mara mbili mfululizo ubingwa wa taji la
ligi kuu bara pamoja na na kombe la FA.
Pia Kaseke alikuwa sehemu ya kikosi cha
Yanga ambacho mwaka 2016 kilitinga hatuna ya robo fainali ya kombe la
shirikisho barani Afrika ambapo kilipangwa kundi moja na timu za TP
Mazembe (Congo),Mo Bejaia (Algeria) na Medeama (Ghana).
0 Maoni:
Post a Comment