
Bingwa mtetezi wa michuano ya
Wimbledon Andy Murray amesukumwa nje ya mashindano hayo na Sam Querrey
katika hatua ya nusu fainali.
Querrey, 29, ameshinda kwa seti 3-6 6-4 6-7 (4-7) 6-1 6-1 na kuwa Mmarekani wa kwanza kufanya hivyo tokea Andy Roddick alipofika katika hatua hiyo mwaka 2009.

Majeraha aliyoyapata pia Novak Djokovic yanamfanya Murray aendelee kushikilia namba moja.
Djokovic namba mbili kwa ubora duniani, alipaswa kushinda mchezo dhidi ya Tomas Berdych lakini majeraha ya kiwiko yakakatisha matumaini hayo.
0 Maoni:
Post a Comment