Wakizungumzia uvamizi huo wahanga wa tukio hilo ambao ni wafanyabashara wamesema kuwa wamesikia milio ya risasi ikisikika majira ya sasa saba usiku katika kijiji hicho na kupigwa butwaa, huku wakiwa kwenye majumba yao wakihofia kuuawa na majambazi hao.
Mwenyekiti wa kijiji cha Nyampande Salum Said Feleshi amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kutaja majina ya watu walioibiwa mali zao na kubainisha kuwa jumla ya mali zilizoibiwa zinathamani ya zaidi ya sh.milioni 3.
Feleshi amesema kuwa uhalifu huo umewachanga kwani katika maduka ya wafanyabiashara hao kulikuwa na walinzi waliowajiri wakiwa na silaha za moto na kusema kuwa tayari walinzi hao wanashikiliwa na Jeshi la Polisi wilayani Sengerema kwa mahojiano zaidi.
0 Maoni:
Post a Comment