Manchester United ni timu yenye jina kubwa,
na kila mchezaji anayecheza katika klabu hii anaaminika kuwa na uwezo
mkubwa, Giggs amempa onyo Lukaku
Ryan Giggs amedai kuwa mchezaji mpya wa Manchester United Romelu
Lukaku atalazimika kuwa mgumu sasa kwa saabu atakuwa akicheza Old
Trafford.
Mshambuliaji huyo wa Everton amejiunga na Mashetani Wekundu dirisha
la uhamisho wa majira ya joto ambao inaaminika walilipa ada ya paundi
milioni 75 kumsajili, na inaweza kuongezeka hadi paundi milioni 90
kutokana na gharama nyingine.
Lukaku, ambaye amefunga mabao 25 Ligi Kuu Uingereza msimu uliopita,
amewahi kuiwakilisha Chelsea, West Bromwich Albion na Everton, lakini
Giggs anaamini presha kubwa itakuwa juu yake akiwa ndani ya fulana ya
United.
“Atapata shinikizo ambalo hajawahi kupata kamwe akiwa West Brom, au Chelsea au Everton,” Giggs alikiambia Sky Sports News.
“Presha itakuwa juu yake. Kwa hiyo anahitaji kuwa na ngozi ngumu,
anahitaji kuwasikiliza makocha, kwa sababu hiyo ndiyo siri pekee, na
ikiwa atapoteza nafasi, mechi itakayofuata atalazimika kurekebisha, kwa
sababu kama mshambuliaji wa kati katika kikosi cha United, presha
inakuwa juu yako muda wote. Nadhani atafunga magoli mengi, lakini
anahitaji kushinda kila mechi.
“Nimemuona kidogo Alvaro Morata; Lakini Lukaku nimemwona zaidi. Faida
ya Lukaku ni kwamba amecheza Ligi Kuu Uingereza na Jose Mourinho
amewahi kufanya naye kazi hapo awali. Ni rafiki wa Paul Pogba, hayo yote
yatamsaidia kuzoea mazingira ya Old Trafford haraka.”
Lukaku amepewa jezi nambari tisa kufuatia kuondoka kwa Zlatan Ibrahimovic.
0 Maoni:
Post a Comment