Mwenyekiti
wa (CUF) anayetambuliwa na ofisi ya Msajili wa Vyama vya siasa, Profesa
Lipumba amefunguka na kusema kuwa Katibu Mkuu wa CUF Mhe. Maalim Seif
Sharif Hamad ana kesi ya kujibu na kudai yeye kawaponza wabunge nane
waliovuliwa uanachama wa CUF
Profesa
Lipumba amesema hayo leo alipokuwa akiongea na waandishi wa habari na
kusema Katibu Mkuu wa (CUF) Mhe. Maalim Seif na yeye anayake ya kujibu
mbele za Kamati ya Maadili na Nidhamu ya CUF.
"Katibu
Mkuu, Naibu Katibu Mkuu na kuna wananchama wengine wengi tu ambao pia
wana makosa ya kuweza kujibu mbele ya Kamati ya Nidhamu na Maadili
katika watu wote hao Katibu Mkuu yumo na yeye ndiye amewaponza hawa
wabunge nane wa Viti Maalum ambao wamevuliwa uanachama na ndugu zangu wa
Zanzibar na wale wabunge wengine wale msiwe mnasikiliza na kufuata kila
anachosema Katibu Mkuu atakuponza kama alivyowaponza wajumbe wa baraza
la wawakilishi" alisema Lipumba
Kwa
upande wa Katibu Mkuu wa CUF Taifa Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad
amesema mpaka sasa wabunge wote nane ambao wanasemakama wamefukuzwa
uanachama wameamua kufungua kesi Mahakama Kuu kupinga maamuzi feki
ambayo yamefanywa na Baraza Kuu feki na kuitaka Mahakama itamke kuwa wao
ni wanachama halali wa CUF na wabunge halali wa Bunge la Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania.
Lakini
pia Katibu Mkuu amesema kuwa Baraza Kuu halali la CUF litakutana kwa
dharura siku ya kesho Ijumaa tarehe 28/07/2017 kujadili mambo mbalimbali
ambayo yanaendelea katika chama hicho na kutangaza hatua ambazo
zitafuata.
0 Maoni:
Post a Comment