Hatua hiyo ya uzinduzi wa gari la zimamoto msaada kutoka kwa Hanspope imekuja punde mara baada ya Gari la jeshi hilo la zimamoto kuanguka na kuharibika vibaya wakati likielekea kuzima moto Isimani wilaya ya Iringa vijijini tarehe 23/04/2017 kwa kukosa muelekea na kuanguka.

Akitoa taarifa wakati wa uzinduzi huo Kamanda wa Jeshi la
zimamoto Kennedy Komba amesema, Mkoa wa Iringa una vituo vya zimamoto vinne
huku kwa jiografia ya mkoa wa Iringa ulitakiwa kuwa na vituo 6 na kwasasa mkoa
una gari moja tu la kuzima moto na la pili ambalo lilipata ajari.
Aidha kamanda amesema katika mkoa wa iringa mwaka 2015-2016
ulikua na matukio ya moto na maokozi takribani 110 ambapo matukio ya moto
yalikua 90 na matukio ya maokozi yalikua 20 ambayo sawa na asilimia 1.1 na
mwaka 2016-2017 matukio ya moto na maokozi yalikua 97 ambapo matukio ya moto yalikua
83 na maokozi yalikua 14 sawa na asilimia 0.97.
Amesema kuna changamoto nyingi zinazoikabili jeshi la
zimamoto kuwa ni mpangilio wa mji hususani nje ya manispaa ya iringa na miundombinu
kwa maana ya barabara . Kamanda amemshukuru Hanspope kwa msaada alioutoa.
Kabla ya kukabidhi Gari hilo lenye uwezo wa kubeba maji lita
5000 ZAKARIA HANSPOPE amesema kwa sasa Manispaa ya Iringa inakua kwa kasi na
hivyo kuna haja kuweza kukabiliana na hali hiyo na majengo makubwa yakiwa
yanajengwa magari kama hayo yanahitajika zaidi kwa usalama wa mali za watu.
“Mimi nimezaliwa hapa Mkoani Iringa na kusoma hapa na baba
yangu pia ameisha hapa hivyo wakati mwingine ni bora kurudisha fadhila kwa mkoa
ambao umetokea kwa kuleta maendeleo. Alisema Hanspope.
Kamishna Jenerali wa zima moto Tanzania Kamanda Thobias
Andengenye ameshukuru kwa kupatiwa msaada huo wa gari na amesema jeshi hilo
lina upungufu wa vifaa vya kuzimia moto na huku vilivyopo pia ni vichakavu.
Amesema katika kutatua changamoto hizo serikali kushirikiana
na jeshi hilo la zimamoto wamekua wakitenga bajeti kwa ununuzi wa vifaa vya
uokozi na kwa mwaka huu wametenga bajeti ya shilingi Bilioni 3 kwaajili ya
kutatua changamoto hiyo.
Kwa upande wake mgeni rasmi Mkuu wa Mkoa wa Iringa Mh Amina
Masenza amemshukuru Hanspope kwa msaada huo na kumuomba kushirikiana nae katika
kutatua matatizo mbalimbali ya kimaendeleo na kwamba mwanzo alishirikiana nae
vizuri wakati timu ya lipuli ilipokosa msaada.
0 Maoni:
Post a Comment