Salah amepewa jezi namba 11 aliyokua akivaa Roberto Firmino ambae kwa sasa atavaa jezi namba 9
Liverpool wamekamilisha dili la usajili winga Mohamed Salah, kutoka As Roma ya Italia, kwa dau la Pauni million 39.
Usajili
wa winga huyu umevunja rekodi ya usajili kwa wachezaji waliowahi
sajiliwa na timu hiyo ambapo usajili wa gharama zaidi ulikuwa wa
mshambuliaji Andy Carrol, aliposajiliwa kwa dau la pauni milioni 35
mwaka 2011.
Salah raia wa Misri mwenye umri wa miaka 25 amesaini mkataba wa miaka mitano kuweza kutumikia Liverpool.
''Ninafuraha
sana kuwepo hapa nitajitoa kwa asilimia mia moja na nitatoa kila kitu
kwa ajili ya klabu hii, kiukweli nataka kushinda kitu nikiwa na timu
hii", alisema Salah baada ya kukamilisha usajili huo.
Ahsante kwa kutembelea site yangu, unaweza kunicheki kwenye mitandao ya kijamii kwa kubonyeza icons juu kulia na kunipata moja kwa moja kwenye Facebook, Twitter na Instagram...Endelea kuwa karibu yangu ili uweze kufikiwa na chochote kinachonifika.
0 Maoni:
Post a Comment