

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimpongeza Anna Elisha Mgwira Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro mara baada ya kumuapisha Ikulu jijini Dar es salaam June 6, 2017
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kassim Majaliwa Majaliwa akimpongeza Anna Elisha Mgwira Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro mara baada ya kuapisha Ikulu jijini Dar es salaam June 6, 2017
Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Anna Elisha Mgwira akiingia kwenye
gari lake kwa ajili ya kwenda kuanza kazi yake Mkoani kilimanjaro mara
baada ya kumuapisha Ikulu jijini Dar es salaam June 6, 2017
Kiapo hicho kinafuatia uteuzi alioufanya Rais Magufuli kwa Mwenyekiti huyo wa chama cha ACT – Wazalendo kuwa Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro mapema mwezi huu.
Mara baada ya kiapo hicho, Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Anna Elisha Mghwira alipanda gari lake la kazini na kuelekea Mkoani Kilimanjaro kuanza kazi rasmi. Mama Anna Mghwira anachukua nafasi ya Said Meck Sadiq ambaye aliomba kujiuzulu na kukubaliwa na Rais Dk John Magufuli.
Mkoa wa Kilimanjaro umepata kuongozwa na wakuu wa mkoa watatu katika kipindi cha miaka miwili, Leonidas Gama ambaye ni mbunge wa Songea Mjini, Said Meck Sadick na Anna Elisha Mghwira.
0 Maoni:
Post a Comment