Nahodha wa Taifa Stars, Mbwana Samatta amesema kwa maandalizi waliyofanya wana uhakika wa kuifunga Lesotho, hivyo amewataka mashabiki wa soka kujitokeza kwa wingi kuwashangilia.
Taifa
Stars baada ya kukaa kambini Misri kwa wiki moja, leo Jumamosi saa 2:00
usiku inacheza na Lesotho mechi ya Kundi L kufuzu Fainali za Kombe la
Mataifa Afrika (Afcon) 2019 kwenye Uwanja wa Azam Complex uliopo Chamazi
nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam.
Kabla
ya mchezo huo, Taifa Stars chini ya Kocha Salum Mayanga huko nyuma
ilicheza mbili za kirafiki na kushinda dhidi ya Botswana na Burundi.
Samatta
anayechezea KRC Genk ya Ubelgiji, amesema wanauchukulia ‘siriazi’
mchezo huo na kikubwa kwao ni kushinda ili kujiwekea nafasi nzuri ya
kufuzu.
“Hii
ni mechi muhimu kwetu, tunaichukulia kwa umakini mkubwa na nia yetu ni
kupata ushindi ambao naamini utatuweka katika nafasi nzuri ya kufuzu.
“Hatuwezi
kuwadharau wapinzani wetu kwa kuwa nao wamejiandaa kwa ajili ya
kupambana na sisi, nawaomba Watanzania waje kutuunga mkono ili tuweze
kufikia malengo yetu,” alisema Samatta.
Kocha
wa Taifa Stars, Mayanga yeye alisema; “Tumejiandaa kushinda na kwa
bahari nzuri tumefanya mazoezi kwenye uwanja wa nyasi bandia na nyasi za
asili, hivyo tutafanya vizuri.”
Akizungumzia
mchezo huo, Kocha wa Lesotho, Moses Malieh, alisema; “Hatukuja kutafuta
sare, tumekuja kupata ushindi na hatutajali wenzetu wanachezaje.”
Kwa
upande wake, nahodha wa Lesotho, Bokang Mothoana alisema: “Tumekuja
kuiwakilisha nchi yetu na malengo yetu ni kupata ushindi kwa sababu
tutacheza kwa kushambulia ili kufikia malengo tuliyojiwekea ingawa
tunawaheshimu wapinzani wetu.”
Taifa Stars itawakosa nyota wake wawili ambao ni majeruhi, Jonas Mkude na Mohammed Hussein ‘Tshabalala’.
0 Maoni:
Post a Comment