KOCHA
Salum Mayanga leo atajaribu kuwa kocha wa kwanza wa timu ya taifa ya
Tanzania, Taifa Stars kushinda mechi tatu mfululizo tangu Marcio Maximo
kati ya 2006 na 2010.
Wadenmark
Jan Polusen na Kim Poulsen ni makocha waliomfuatia Maximo na chini yao
Taifa Starsv haikuwahi kushinda mfululizo zaidi ya mechi mbili, kama
ilivyokuwa kwa Mholanzi Mart Nooij na mzalendo mwingine, Charles
Boniface Mkwasa.
Mayanga
leo ataiongoza Taifa Stars katika mchezo wa kwanza wa Kundi L kufuzu
Kombe la Mataifa ya Afrika mwaka 2019 nchini Cameroon, itakapomenyana na
Lesotho kuanzia Saa 2:00 usiku Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es
Salaam
Ataiingiza
timu uwanjani leo ikitoka kushinda mechi mbili mfululizo za kirafiki
mwezi Machi, 2-0 dhidi ya Botswana na 2-1 dhidi ya Burundi.
Na ikumbukwe Taifa Stars inaingia katika mchezo wa leo ikitoka kuweka kambi ya wiki moja nchini Misri katika Jiji la Alexandria.
Mchezo
huo umelazimika kupelekwa kwenye Uwanja wa klabu ya Azam FC kutokana
Uwanja wa Taifa kuwa katika ukarabati mdogo na Shirikisho la Soka
Tanzania (TFF) limeahidi ulinzi mkali ndani na nje kuhakikisha mambo
hayaharibiki leo.
Mayanga
amewapata wachezaji wote wa Ulaya, kuanzia Nahodha Mbwana Samatta wa
KRC Genk ya Ubelgiji, mshambuliaji mwenzake wa zamani wa TP Mazembe ya
DRC, Thomas Ulimwengu wa AFC Eskilstuna ya Denmark na winga Farid Mussa
wa DC Tenerife ya Hispania.
Na
kwa hapa nyumbani amewarudisha nyota wote aliowatumia kwenye mechi za
Machi dhidi ya Botswana na Burundi, wakiwemo chipukizi washambuliaji
Mbaraka Yussuf Abeid na Abdulrahman Mussa.
Amemtema
tu kipa Deo Munishi ‘Dida’ na kumchukua mchezaji mwenzake wa Yanga,
Benno Kakolanya – na maana yake leo anaweza akadaka Aishi Manula wa Azam
FC. Kipa mwingine ni Said Mohammed Mduda wa Mtibwa Sugar.
Mayanga,
muumini wa mfumo wa 4-4-2 kikosi chake leo kinaweza kuwa; Aishi Manula,
Shomary Kapombe, Mwinyi Mngwali, Abdi Banda, Salim Mbonde, Himid Mao,
Muzamil Yassin, Salum Abubakar ‘Sure Boy’, Mbwana Samatta, Thomas
Ulimwengu na Farid Mussa.
Katika
benchi watakuwapo; Said Mohammed, Hassan Kessy, Aggrey Morris, Erasto
Nyoni, Said Ndemla, Simon Msuva, Shiza Kichuya, Mbaraka Yussuf, Ibrahim
Hajib na Abdulrahman Mussa.
Kila la heri Taifa Stars. Mungu ibariki Tanzania. Amin.
0 Maoni:
Post a Comment