Mfungaji wa mabao mawili ya England Dominic Solanke katikati akishangailia na wachezaji wenzake
Timu za England na Venezuela
zimetinga kwenye hatua ya fainali ya michuano ya kombe la dunia la
vijana chini ya umri wa miaka 20.
England wametinga katika hatua
ya fainali kwa kuichapa Italia kwa mabao 3-1 magoli ya England yamefugwa
na Dominic Solanke aliyefunga mara mbili na Ademola Lookman huku goli
pekee la Italia likifungwa na Riccardo Orsolini.
Katika mchezo
mwingine wa nusu fainali Venezuela wamewachapa Uruguay kwa mikwaju ya
penati 4-3 baada ya sare ya goli 1-1 katika dakika tisini za kwaida.
Mchezo
wa fainali kati ya England na Venezuela utachezwa june 11 katika
dimba la Suwon mchezo huo ukitanguliwa na mchezo wa mshindi wa tatu
kati ya Italia na Uruguay.
Ahsante kwa kutembelea site yangu, unaweza kunicheki kwenye mitandao ya kijamii kwa kubonyeza icons juu kulia na kunipata moja kwa moja kwenye Facebook, Twitter na Instagram...Endelea kuwa karibu yangu ili uweze kufikiwa na chochote kinachonifika.
0 Maoni:
Post a Comment