Meya
wa Jiji la Arusha, Calist Lazaro ametoa siku saba kwa Mkuu wa Mkoa wa
Arusha, Mrisho Gambo amuombe radhi kwa kosa la kumuweka ndani wakati
alipokuwa anakabidhi rambirambi kwa wazazi waliofiwa kwenye ajali ya
gari la Shule ya Msingi Lucky Vincent.
Akiongea
na waandishi wa habari ofisini kwake jana Ijumaa, Lazaro alisema mpaka
sasa ameshindwa kuelewa ni kwanini mkuu huyo aliagiza meya pamoja na
wenzake wakiwemo viongozi wa dini, madiwani, wawakilishi waliotoa
rambirambi na mwenye shule kukamatwa na Jeshi la Polisi na kuwekwa
ndani.
"Mimi
sikuwa na shida na RC na kitendo cha kumuweka ndani kiongozi wa dini,
paroko, kiongozi wa dini ya Kiislamu ni kitendo ambacho si cha
kibinadamu na anapaswa aombe radhi umma,"alisema.
Pia,
alimtaka kutafakari nafasi yake na kuona kuwa anafaa kuendelea kuwa
mkuu wa Mkoa wa Arusha kwasababu ameonyesha kuwatumikia wananchi ambao
hawaheshimu.
"Hana heshima na mbunge, madiwani, watu wenye degree zao, haheshimu viongozi wa dini halafu bado anataka uongozi,"alisema.
0 Maoni:
Post a Comment