Chama cha soka nchini Uingereza FA
kimesema kitaanzisha sheria mpya kwa wachezaji wanaojirusha hovyo
uwanjani ama wale wanaodanganya kuumia wakati wa mchezo ili kupoteza
muda.
FA imesema kuwa jopo la wataalam litakaa kujadili namna ya kushughulikia suala hilo, huku tukio zima likirudiwa kutizamwa na mwamuzi, meneja wa timu pamoja na mchezaji mwenyewe kabla ya kutolewa kwa hukumu.
Kama kila mmoja ataridhishwa juu ya mbinu za uongo zilizotumiwa, mchezaji husika atafungiwa michezo miwili.
0 Maoni:
Post a Comment