CCM yalia na mauaji Kibiti

Chama Cha Mapinduzi (CCM), kimesema kuwa kimehuzunishwa na kimesikitishwa sana na mauaji yanayoendelea eneo la Mkuranga, Kibiti na Rufiji mkoani Pwani. 
 
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es salaam, Alhamisi hii , Katibu wa wa itikadi na uenezi (CCM) Humphrey Polepole, ameonyeshwa kusikitishwa na matukio hayo.

“Suala la ulinzi na usalama wa Wananchi wetu wa Tanzania hasa zaidi katika muendelezo wa matukio kwenye eneo la Mkuranga, Kibiti na Rufiji. Sisi kama chama tumelifuatilia na tumeona ni vyema kusimama na Watanzania wakiwemo Wanachama wa CCM katika maeneo haya kusema tuko pamoja, tunatambua wanapitia wakati mgumu, tunatambua maisha ya wananchi wetu, Watanzania wetu, watendaji wetu, wapo askari wetu, wapiganaji wetu,” alisema Polepole.

“Lakini pia wapo wanachama wenzetu wa chama cha Mapinduzi, wapo viongozi wetu wa Chama cha Mapinduzi,” alisema Polepole.Wapo waliopoteza maisha sio kwasababu ya mapenzi ya Mwenyenzi Mungu wamepoteza maisha yao kwasababu yamekatizwa katika namna ambayo inakiuka kila namna ya ubinadamu na wameuawa kikatili na watu ambao hawana mioyo hawana hisia hawana mioyo hata kidogo.”

Aidha Polepole aliongeza kuwa “Chama cha Mapinduzi kimehuzunishwa sana, kinasikitishwa sana, tumeumia sana naomba niseme kwa niaba ya Mwenyekiti wetu wa Chama cha Mapinduzi naomba niseme kwa niaba ya Katibu Mkuu wetu na uongozi mzima wa Chama cha Mapinduzi tumehuzunishwa sana tena sana.”
Share on Google Plus
Ahsante kwa kutembelea site yangu, unaweza kunicheki kwenye mitandao ya kijamii kwa kubonyeza icons juu kulia na kunipata moja kwa moja kwenye Facebook, Twitter na Instagram...Endelea kuwa karibu yangu ili uweze kufikiwa na chochote kinachonifika.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 Maoni:

Post a Comment