Shirika
la Umeme Tanzania (TANESCO) limetoa siku 14 kwa Shirika la Visiwani
Zanzibar (ZECO) kulipa deni lote la ankara za umeme wanalodaiwa na
endapo halitafanya hivyo basi hatua kali za kisheria zitachukuliwa ikiwa
ni pamoja na kukatiwa umeme.
Kauli
hiyo imetolewa leo na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa shirika hilo Dkt.
Tito Mwinuka alipokuwa anaongea na waandishi wa habari Jijini Dar es
Salaam ambapo amesema hadi kufikia mwezi Januari mwaka 2017, Shirika la
Umeme Zanzibar (ZECO) lilikuwa linadaiwa zaidi ya shilingi bilioni
127.8.
“Shirika
la umeme linashindwa kutekeleza majukumu yake mbalimbali kwa wakati
ikiwemo uendeshaji wa shirika, matengenezo ya miundombinu pamoja na
utekelezaji wa miradi, hayo yote yanasababishwa na malimbikizo ya madeni
kwa wadaiwa sugu hivyo tunatoa siku 14, wasipoweza kulipa tutawakatia
huduma ya umeme”. Alisema Dkt Mwinuka
Aidha
mbali na ZECO, Tanesco imewataja wadaiwa sugu wengine ikihusisha Wizara
na Taasisi za serikali zikiwa zinadaiwa zaidi ya bilioni 52.5,
makampuni binafsi pamoja na wateja wadogo wanaodaiwa zaidi ya bilioni
94.9
Kwa
upande mwingine Dkt. Mwinuka amesema shirika hilo linatarajia kuanza
oparesheni maalum ya kukusanya madeni hayo na matarajio yao ni kulipwa
kwa malikimbizo yote ili yalisaidie kujiendesha kiushandani na kwa
ufanisi mkubwa zaidi na kuchochea kasi ya ukuaji sekta mbalimbali
zinazotegema nishati ya umeme nchini.
Hatua
hii imekuja ikiwa ni takriban siku 4 tangu Rais Magufuli kuagiza
TANESCO kufuatilia madeni yote ikiwemo deni ambalo TANESCO inalidai
ZECO, na kuitaka kuwakatia umeme wote watakaoshindwa kulipa kwa wakati.
0 Maoni:
Post a Comment