Mfanyabiashara maarufu Yusufu Manji amepata dhamana baada ya kusomewa shtaka moja la kutumia dawa za kulevya aina ya heroine.
Manji
amesomewa shtaka hilo katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu baada ya
wakili wake Alex Mgongolwa kuiomba dhamana na Jamhuri kusema haina
pingamizi kwani shtaka hilo linadhaminika.
Hakimu
Cyprian Mkeha amesema Manji atakuwa nje kwa dhamana kwa sharti la
kusaini bondi ya dhamana ya Sh10 milioni na awe na mdhamini mmoja
ambaye atasaini bondi ya Sh10 milioni.
Amedhaminiwa na Katibu Mkuu wa Yanga Charles Mkwassa.Kesi itasikilizwa tena March 16
0 Maoni:
Post a Comment