Ulinzi waimarishwa Taasisi ya Moyo Muhimbili Ambako Yusuf Manji amelazwa


 
Hali ya ulinzi imeimarishwa katika Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) alikolazwa mfanyabiashara Yusuf Manji baada ya kuugua ghafla akiwa polisi alikokuwa akihojiwa.

Manji aliyekuwa akihojiwa katika Kituo Kikuu cha Polisi jijini hapa alipelekwa hospitalini hapo juzi jioni akiwa ndani ya gari la wagonjwa aina ya Toyota Land Cruiser lenye nembo ya Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi (UNHCR) huku gari lake aina ya Range Rover likifuata kwa nyuma.

Askari wenye sare na wengine wakiwa na mavazi ya kiraia nje ya wodi aliyolazwa mwenyekiti huyo wa klabu maarufu nchini ya Yanga walionekana wakiimarisha ulinzi.

Ilipofika saa 4:13 asubuhi mfanyabiashara huyo alitoka kwenye chumba hicho na kuongozwa kuelekea upande mwingine wa jengo hilo.

Akiwa amevalia nguo za wagonjwa zenye rangi ya kijani, Manji alitembea taratibu kuelekea upande aliokuwa akielekezwa.

Alipoulizwa kuhusu uwapo wa Manji hospitalini hapo, Mkurugenzi Mtendaji wa JKCI, Profesa Mohamed Janabi alisema hawezi kuzungumzia taarifa za mgonjwa.

Februari 8, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda alitoa orodha ya watu 65, akiwamo Manji ambao aliwataka wafike Polisi kwa ajili ya mahojiano kuhusu masuala ya dawa za kulevya.
Share on Google Plus
Ahsante kwa kutembelea site yangu, unaweza kunicheki kwenye mitandao ya kijamii kwa kubonyeza icons juu kulia na kunipata moja kwa moja kwenye Facebook, Twitter na Instagram...Endelea kuwa karibu yangu ili uweze kufikiwa na chochote kinachonifika.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 Maoni:

Post a Comment