Mbunge
wa Singida Mashariki, Tundu Lissu, amemtaka Kamanda wa Polisi Mkoa wa
Kipolisi Ilala, Kamishna Msaidizi wa Polisi, Salum Hamdani, kueleza
anachofahamu juu ya Katiba ya Zanzibar na kama Mwenyekiti wa Tume ya
Uchaguzi Zanzibar , Salum Jecha ana mamlaka ya kufuta matokeo ya
uchaguzi au laa.
Lissu
alihoji hayo jana katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu mbele ya
Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba, wakati Hamdani alipokuwa akitoa
ushahidi katika kesi ya uchochozi inayomkabili Lissu na wahariri wa
Gazeti la Mawio.
Mshtakiwa
Lissu aliomba kujiwakilisha mwenyewe mahakamani hivyo baada ya ushahidi
alimuhoji maswali shahidi kulingana na ushahidi wake.
Swali
hilo la Lissu lilimfanya Wakili wa Serikali, Paul Kadushi, kupinga
akitaka shahidi asijibu kwa sababu si mtaalamu wa sheria wala Katiba.
Kadushi
alidai shahidi hawezi kutoa tafsiri ya Katiba ya Zanzibar na Mahakama
ya Hakimu Mkazi Kisutu haina mamlaka ya kusikiliza masuala ya kikatiba.
Akijibu
pingamizi hilo, Lissu alidai halina msingi wowote kwa sababu suala la
Serikali ya Zanzibar ni halali na limeletwa na upande wa mashtaka
wenyewe katika shtaka la pili na la tatu hivyo wakabiliane nalo.
Wakili
Peter Kibatala alidai mahakamani hapo kuwa shahidi huyo anapaswa
kueleza yeye mwenyewe kama hawezi kulijibu swali hilo na si vinginevyo
na kwamba katika kuandika uamuzi wake mahakama ipende isipende ni lazima
itajibu swali hilo.
Hakimu
Simba baada ya kusikiliza hoja za pande zote mbili aliahidi kutoa
uamuzi leo iwapo shahidi aeleze anachokifahamu kuhusu Katiba ya Zanzibar
ama la.
Kabla ya kufikia katika malumbano hayo Lissu alitaka kujua yeye na washtakiwa wenzake walikula wapi kuchapisha huo uchochezi.
Alihoji
wao watu wanne waliwasiliana kwa maandishi, email ama simu na saa
ngapi, maswali hayo yalijibiwa na shahidi kwamba hafahamu.
Awali
akihojiwa na Wakili Kibatala kuhusu wapi alipata taarifa za kuwapo kwa
mikusanyiko ya watu katika sehemu za kuuzia magazeti , Hamdani alidai
alizipata kwa RCO wa Kinondoni, Temeke na Ilala na kwa upande wa
Zanzibar alipata kutoka kwa aliyekuwa Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa
ya Jinai (DCI), Diwani Athumani.
Shahidi
alidai katika Gazeti la Mawio la Januari 14 mpaka 20 kulikuwa na habari
yenye kichwa cha habari Machafuko yaja Zanzibar na kwamba maneno hayo
yangeweza kuleta chuki, uvunjifu wa amani, uchochezi na hofu.
Alidai
baada ya kuona hivyo na kulinua gazeti hilo alifungua jalada la
uchunguzi kisha aliteua wapelelezi ili kuona kama kuna kesi ya jinai na
walipoona waliwafikisha washtakiwa mahakamani.
0 Maoni:
Post a Comment