Kati ya makocha waliopo katika wakati mgumu kwa sasa Arsene Wenger anaongoza.Matokeo mabovu ndani ya ligi Uingereza yamewachosha mashabiki na kuanza kumshambulia Mfaransa huyo.Achilia mbali kinachomtokea Wenger katika ligi ya Uingereza lakini kipigo mujarabu katika ligi ya klabu bingwa Ulaya kimemfanya Wenger azidi kuwa na wakati mgumu.
Huku mashabiki wa Arsenal wakishinikiza Wenger
aondoke,Wenger mwenyewe ana uhakika wa kuwa kocha msimu ujao.Japokuwa
Wenger hajasema moja kwa moja kwamba atakuwa kocha wa Arsenal msimu ujao
lakini Mtandao huu unaelewa kwamba mkataba wa miaka miwili mingine upo mezani kwake na ataamua mwenyewe kusaini au kuacha ila kufukuzwa ni ngumu.
“Sina mashaka kuhusu msimu ujao,nina uhakika
nitakuwa kocha wa hapahapa au mahala pengine,kwa sasa nina mambo ya
kuangalia lakini sio kuhusu maisha yangu ya mbeleni,inabidi kwanza
tuangalie nini kitapatikana hadi mwisho wa msimu huu inabidi niiangalie
zaidi Arsenal na sio mimi kama mimi” alisema Wenger.
Wenger hapo mwanzo aliwahi kusema kati ya mwezi wa tatu
au wanne atatoa maamuzi yake kuhusu uwepo wake katika timu hiyo.Lakini
Wenger sasa anasema hakumaanisha hivyo ila alitaja mwezi wa tatu au
wanne kwakuwa yeye binafsi hajui ni lini atato maamuzi kuhusu
mustakabali wake na Arsenal.
Wenger pia amekanusha habari zilizosambaa kwamba
kulikuwa na ugomvi katika vyumba vya kubadilishia nguo katika safari yao
ya Ujerumani.Kuhusu maoni ya bodi ya timu juu yake Wenger amesisitiza
kwamba lazima bodi ifanye maamuzi sahihi ya kuisaidia Arsenal sii tu kwa
sasa bali pia huko mbeleni.“Mwanzoni sikudhani kama naweza
kukaa hapa kwa miaka 20,nilipata nafasi sehemu mbali mbali lakini
mapenzi yangu na timu hii ndio maana hadi sasa niko hapa” alisema Wenger.
“Hata nikiondoka Arsenal haitaishinda mechi
zote,kwanza wakati nakuja hapa walikuwa wana mechi chache za UEFA kuliki
baada ya mimi kuja hapa,mimi sio mtu wa kwanza kushindwa kubeba UEFA na
Arsenal,nilipokuja hapa pia hawakuwa na hilo kombe” alimalizia Wenger.
0 Maoni:
Post a Comment