Mtazamo wa Shaffih Dauda kuelekea Simba vs Yanga



Zikiwa zimesalia siku 4 kufikia pambano la watani wa jadi Simba vs Yanga, tayari joto la mechi hiyo limeshapanda huku gumzo la mjini likiwa ni kuwa, mshindi wa mchezo huo atakuwa na nafasi kubwa ya kutwaa taji la ligi kuu Tanzania bara kwa msimu huu.

Tayari vilabu hivyo vipo kambini kujiandaa na game hiyo ambayo ndio inatajwa kuwa mechi kubwa ambayo inafatiliwa na watu wengi zaidi nchini.

Shaffih Dauda mchambuzi wa masuala ya michezo wa Clouds Media Group ametoa mtazamo wake kuelekea mchezo huo ambapo amesema kuwa, mshindi wa game ya watani wa jadi siku ya Jumamosi ijayo atajiweka kwenye nafasi nzuri ya kutwaa ubingwa wa taji la VPL.

“Kwa siku za hivi karibuni kushuhudia mechi ya Simba vs Yanga imekuwa inatokea huku timu hizo zikiwa zimeachana kwa pointi nyingi kwenye msimamo wa ligi tofauti na mechi ijayo ya February 25 ambapo timu hizo zinafatana kwenye msimamo wa ligi zikitofautishwa na mbili Simba ikiwa inaongoza ligi kwa pointi 51 wakati Yanga wao wana pointi 49 katika nafasi ya pili,” – Shaffih Dauda.

“Timu hizi kuna wakati zilikuwa zinakutana kwenye mechi ya watani wa jadi zikiwa zinafatana lakini unakuta ni kwa nafasi ya pili na ya tatu au zikiwa hazifatani, unakuta timu mmoja ipo nafasi ya kwanza nyingine pio katika nafasi ya tatu lakini safari hii zinakutana zikiwa nafasi ya kwanza na ya pili  tena zikiwa zinatofautishwa kwa pointi mbili.”

“Kwa hiyo mechi ijayo itakuwa na presha mara mbili, achilia ile presha ya upinzani wa kawaida lakini kutakuwa na presha ya kupata matokeo kwa sababu ni mechi hiyo muhimu kwa kila timu ‘lazima kila timu ipate ushindi’ wenzetu wanasema ‘a must win match’ kwa sababu matokeo ya ushindi yanaitengenezea kila timu mazingira ya kuchukua ubingwa wa ligi kuu Tanzania bara.”

“Mechi hiyo itakuwa na presha zaidi kwa Simba kwa sababu wanajua fika kwa namna walivyoanza ligi msimu huu hadi walipo sasa hivi ndio msimu ambao wana nafasi kubwa ya kuchukua ubingwa, kwa hiyo wakiifunga Yanga ambayo ndio timu inayoonekana kuwa na upinzani mkubwa kwa sasa kwenye mbio za ubingwa, watakuwa wanatengeneza mazingira ya kukimbia zaidi kwenda kuchukua ubingwa wa VPL ambao wameukosa kwa muda mfupi.”
Share on Google Plus
Ahsante kwa kutembelea site yangu, unaweza kunicheki kwenye mitandao ya kijamii kwa kubonyeza icons juu kulia na kunipata moja kwa moja kwenye Facebook, Twitter na Instagram...Endelea kuwa karibu yangu ili uweze kufikiwa na chochote kinachonifika.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 Maoni:

Post a Comment