Idara
ya Uhamiaji Mkoa wa Dar es Salaam imesema inakusudia kumfungulia
mashtaka mfanyabiashara maarufu Yusufu Manji kwa kosa la kuajiri
wafanyakazi wageni 25 wasiokuwa na vibali vya kufanya kazi nchini
kupitia Kampuni ya Quality Group.
Katika
taarifa hiyo Manji alisema baada ya kustaafu atabakia kuwa mshauri huku
akitaja sababu za kufanya hivyo kuwa ni utaratibu uliokuwa umewekwa na
waasisi wa kampuni hiyo wa kuwa na ukomo wa uongozi usiozidi miaka 20.
Katika
taarifa hiyo alieleza kuwa ameshatumikia nafasi hiyo kwa miaka mingi na
ni muhimu kutoa fursa kwa kiongozi mwingine ili aweze kujishughulisha
na shughuli nyingine ikiwamo kufundisha katika vyuo vikuu ujasiriamali.
Akizungumza
Dar es Salaam jana, Kamishna wa Idara hiyo, John Msumule alisema kazi
hiyo itafanyika baada ya mfanyabiashara huyo kutoka hospitali alikolazwa
akiendelea na matibabu ambapo ataunganishwa na kesi hiyo na lazima
afikishwe mahakamani.
“Jumla
ya wafanyakazi walikuwa 128, kati yao wawili walikimbia nchi na kubaki
126 na baada ya ukaguzi tuliwabaini wengine 25 wakiwa hawana vibali vya
kufanya kazi nchini.
“Taratibu
zetu ni kuwafungulia mashtaka waliokamatwa lakini pia tutamfikisha
mahakamani muajiri wao kwa kufanya makosa hayo huku akijua ni kinyume na
sheria,” alisema Musumule.
Alisema
walianza kufanya ukaguzi katika kampuni hiyo Ijumaa ya wiki iliyopita
lakini hawakupewa ushirikiano ambapo walimkamata msaidizi wake.
“Siku
ya Jumamosi walikuwa na passport hapa lakini wafanyakazi wawili
walikimbia nchi na ndipo tulipogundua kuna 25 wanaofanya kazi katika
kampuni hiyo bila kuwa na kibali,”alisema Musumule.
Mbali
na hilo alisema wamefanikiwa kumkamata raia wa Uganda, Asha Talib
ambaye alikuwa na makosa ya kuishi nchini bila kibali, kuhondhi hati za
kusafiria 15 za raia wa Uganda na tatu za Madagaska.
Mtuhumiwa
huyo alipokuwa akihojiwa mbele ya waandishi wa habari alidai kuwa
alikuwa anafanyakazi katika kampuni inayoshughulika na maombi ya viza
kwa njia ya mtandao ambapo bosi wake raia wa Tanzania alikimbia.
“Kazi
tuliyokuwa tunafanya ni kuwapatia watu mbalimbali viza baada ya kufanya
maombi kwa njia ya mtandao na kisha kuwatumia viza hizo za kusafiria
huko waliko,” alisema Talib.
Aidha
katika hatua nyingine Kamishna Musumule alisema kuwa kuna baadhi ya
watumishi wa idara hiyo wasiokuwa waminifu ambao wamekuwa wakishiriki
katika kughushi hati mbalimbali za kusafiria.
“Wiki
ijayo nendeni Makao Makuu ya Idara ya Uhamiaji ambapo tutawatangazia
hatua ambazo tumezichukua juu ya watumishi hao ambao si
waaminifu,”alisema Musumule.
Alisema
katika operesheni hiyo, walikamata vibali bandia nane vya raia wa
China wa Kampuni ya Global Leader na ukaguzi uliofanyika katika jengo la
Diamond Plaza walibaini Kampuni ya Luck Spin.
“Pia
tumefanikiwa kumkamata mwajiri raia wa Tanzania kwa kumwajiri mgeni
kutoka nchini Malawi katika kampuni ya ulizi kinyume cha sheria,”
alisema Musumule.
0 Maoni:
Post a Comment