Jeshi
la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limetoa taarifa ya kukamatwa
kwa jumla watuhumiwa 349 katika oparesheni ya kuwasaka watu wanaohusika
na dawa za kulevya
Akizungumza
leo Jijini Dar es Salaam, Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es
Salaam, Kamishna Simon Sirro amesema kati ya watuhumiwa hao, wamo
wauzaji, wasafirishaji na watumiaji wa dawa za kulevya, na kwamba
wataanza kufikishwa mahakamani siku ya kesho, huku mmoja akipandishwa
kizimbani leo.
Pia
ametoa taarifa ya kijana mmoja anayedaiwa kusambaza taarifa za uongo,
ambapo amesema kuwa jeshi hilo linamshikilia kijana huyo ambaye ni
mwanafunzi mwenye umri wa miaka 23, anayedaiwa kutaja majina ya viongozi
na kuwatuhumu kuwa wanahusika na dawa na dawa za kulevya.
Kuhusu
askari 9 waliotuhumiwa kuhusika na dawa hizo, Kamanda Sirro amesema
askari hao wamekabidhiwa kwa Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya kuzuia na
Kupambana na Dawa za Kulevya kwa ajili ya kuchukuliwa hatua za kisheria.
Kamanda
Sirro amesema hadi sasa jumla ya kete 612 pamoja na bangi vimekamatwa
na kwamba kuna watu wengine 17 ambao bado jeshi hilo linawafuatilia na
watakuwa mbaroni wakati wowote.
0 Maoni:
Post a Comment