Unaikubali simu yako ya Tecno? Shinda safari ya Uingereza ukajiachie na supastaa



xmass-campaign
Kampuni ya simu ya Tecno hii leo imezindua kampeni ya Christmas ambayo
inawawezesha wateja wake kujishindia tiketi za safari ya kuzuru nchini
Uingereza katika kampeni inayokwenda kwa jina la #KamaMbele.  


Uzinduzi huu ni katika jitihada za Tecno kuwapatia wateja wake zawadi
katika msimu huu wa Sikukuu za Christmas na Mwaka Mpya na kuwawezesha
kununua simu bora kwa gharama nafuu hivyo kuwawezesha kufurahia pamoja.
Mwanadada mrembo anayeng’arisha video za mastaa wa Bongo (Video Vixen),
Hamisa Mobetto na Mshindi wa Big Brother Africa – Hotshots mwaka 2014,
Idris Sultan ni mabalozi wa kampeni hii ambapo mmoja wao ( Idris au
Hamisa) atashinda safari ya Uingereza akiambatana na shabiki mmoja.



Jinsi ya kushiriki ni kwamba mteja ataingia kwenye tovuti ya shindano
ambayo ni http://tecnokamambele.co.tz/ atapiga kura kwa supastaa moja
kati ya Idris au Hamisa kisha ataeleza kwanini anaikubali Tecno yake
akitumia hashtag #KamaMbele na shabiki mshindi atapatikana kutokana na
kura zitakazopigwa na mashabiki katika hatua ya pili ya shindano.



Mbali na kujishindia safari ya kwenda nchini Uingereza, wateja wa
Tecno na Watanzania kwa ujumla wataweza kujishindia zawadi mbalimbali na
kupata punguzo la bei katika simu za Tecno. 




Endapo ungependa kusafiri na Hamisa Mobeto tazama video hii kisha ingia http://tecnokamambele.co.tz/ kumpigia kura. 


Share on Google Plus
Ahsante kwa kutembelea site yangu, unaweza kunicheki kwenye mitandao ya kijamii kwa kubonyeza icons juu kulia na kunipata moja kwa moja kwenye Facebook, Twitter na Instagram...Endelea kuwa karibu yangu ili uweze kufikiwa na chochote kinachonifika.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 Maoni:

Post a Comment