Ronaldo kakubali kusaini mkataba utaomuweka Madrid hadi akifikisha miaka 36

Cristiano Ronaldo
Cristiano Ronaldo amejipiga pingu baada ya kukubali kuongeza mkataba mpya utakao mbakiza Real Madrid hadi  June 2021.
Nyota huyo mwenye miaka 31 kwa sasa, mkataba wake wa sasa unamalizika June 2018 lakini Ronaldo ambaye ni nahodha wa Ureno atasaini mkataba mpya Jumatatu (leo) utakaomalizika akiwa na miaka 36.
Inaripotiwa kwamba, mshahara wa Ronaldo kwa wiki utaendelea kubaki £365,000.
Ameshafunga magoli 371 tangu alipojiunga na Madrid akitokea Manchester United mwaka 2009.
Mshambuliaji huyo wa Ureno ameisaidia Madrid kushinda taji la Champions League mara mbili taji moja la La Liga tangu alipohamia makao makuu ya Hispania miaka saba iliyopita.
Real Madrid walitoa taarifa yao inayosema kwamba Ronaldo atasaini makataba mpya wa kusalia Bernabeu tangazo ambalo limekuja wiki moja baada ya mchezaji mwenzake Gareth Bale kuongeza mkataba hadi mwaka 2022 na miaka hiyo ya soka la Hispanaia.
Ronaldo alikisaidia kikosi cha Madrid kupaa hadi nafasi ya kwanza La Liga baada ya ushindi wa 3-0 dhidi ya Laganes siku ya Jumapili.
Baada ya mchezo, kocha wa Real Madrid Zinedine Zidane alimsifia Ronaldo kwa kusema ni mchezaji wa kipekee.
Zidane aliongeza: “Ni ndo yake kumaliza maisha yake ya soka akiwa hapa.”
“Ninafuraha kwamba anaweza kuongeza mkataba na kumaliza soka lake akiwa anavaa jezi nyeupe kama nilivyofanya miaka mingi iliyopita.”
Share on Google Plus
Ahsante kwa kutembelea site yangu, unaweza kunicheki kwenye mitandao ya kijamii kwa kubonyeza icons juu kulia na kunipata moja kwa moja kwenye Facebook, Twitter na Instagram...Endelea kuwa karibu yangu ili uweze kufikiwa na chochote kinachonifika.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 Maoni:

Post a Comment