Cristiano Ronaldo amefunga hat-trick yake ya 39 iliyoipa Real Madrid ushindi kwenye mchezo wa Madrid derby dhidi ya mahasimu wao Atletico Madrid na kuwafanya waongoze kwenye msimamo wa La Liga
Raia huyo wa Ureno alainza kufungua nyavu za Atletico kwa mkwaju wa free-kick uliomgonga beki wa Atletico na kumpoteza maboya golikipa Jan Oblak.
Ronaldo aliongeza bao la pili kwa mkwaju wa penati kabla ya kukamilisha hat-trick yake alipounganisha krosi ya Gareth Bale.
Real wanaongoza kwenye msimamo wa La Liga kwa pointi zaidi ya wapinzani wao Barcelona ambao wako nafasi ya pili baada ya kung’ang’aniwa na Malaga kwa kulazimishwa suluhu kwenye uwanja wa Camp Nou.
Ronaldo ameshafunga magoli nane ndani ya La Liga msimu huu na kuwafikia ma-star wa Barcelona Lionel Messi pamoja na Luis Suarez.
Nyota huyo mwenye miaka 31 pia amevunja rekodi ya legendary wa Real Alfredo Di Stefano ambaye alifunga magoli 17 kwenye mchezo wa Madrid derby baada ya mshindi huyo wa Euro 2016 kufikisha mabao 18 kwenye mchezo wa mahasimu wa jiji moja. Magoli 18 aliyofunga Ronaldo dhidi ya Rojiblancos, ni magoli mengi zaidi kuliko mchezaji yeyote kwenye historia kwa sasa.
Cristiano Ronaldo sasa amefunga hat-trick 39 akiitumikia Real Madrid pekee huku aiwa ameshafunga hat-trick 44 katika maisha yake ya soka la ushindani huku ikiwa ni hat-trick ya pili katika uwanja wa Vicente Calderon dhidi ya Atletico Madrid.
0 Maoni:
Post a Comment