Tottenham Hotspur wameendelea kuudhihirishia ulimwengu namna gani michuano mikubwa kama Ligi ya Mabingwa Ulaya si saizi yao licha kuwa na kikosi bora msimu huu.
Kwa mara nyingine tena wameshindwa kupanda mlima ambao haukuwa na vikwazo vikubwa ukilinganisha na milima mingine.
Baada ya kupitia nyakati nzuri msimu uliopita kabla ya kushindwa mbio za ubingwa wa EPL na baadaye kuzidiwa kete na mahasimu wao wa London Arsenal katika nafasi ya pili, vijana hao wa Mauricio Pochettino wameshindwa kufuzu hatua ya 16 bora ya Ligi ya Mabingwa baada ya kupokea kipigo cha mabao 2-1 kutoka kwa Monaco.
Licha kushuhudia Radamel Falcao akikosa penati na kuona Harry Kane akiifunga goli, Tottenham hawakuweza kufua dafu mbele ya Wafaransa hao na hatimaye kutupwa nje ya michuano hiyo yenye hadhi kubwa zaidi kwa vilabu barani Ulaya.
Wakiwa juu kwa alama moja dhidi ya CSKA Moscow, timu hiyo yenye maskani yake London ya kaskazini hawatakuwa tayari kupoteza mchezo wao wa mwisho.
Lakini hiyo si sababu ya watu kutowasema vibaya mitandaoni. Hivi ndivyo watu walivyowananga kupitia Twitter baada ya kutupwa nje.
When you ask a Spurs fan about the Champions League… pic.twitter.com/SoDSZBKWPO— Together Arsenal (@TogetherArsenal) November 22, 2016
Spurs fans returning home like… pic.twitter.com/tVogtADfAJ— TheFootballCommunity (@Footy_Community) November 22, 2016
See you later Spurs!#THURSDAYNIGHT pic.twitter.com/X1dVQWy02u— ArsenalFanTV (@ArsenalFanTV) November 22, 2016
0 Maoni:
Post a Comment