Siku kadhaa zilizopita mchezaji wa Manchester City anayekipiga kwa mkopo Sevilla, Samir Nasri alinukuliwa akisema kuwa kocha wa Man City, Pep Guardiola amewakataza wachezaji wake kufanya mapenzi usiku.
Alisema sababu ya kufanya maamuzi hayo ni kuhofia wachezaji kupata majeraha ya mara kwa mara lakini pia kupata muda wa kutosha wa kumpumzika hata kama siku inayofuatia ni mapumziko.
Kufuatia kauli hiyo, Kocha Guardiola amezungumza kuhusu alichokisema Nasri na kusema kuwa ni kweli kwani ni muhimu wa mchezaji kufanya mapenzi na mwenza wake.
“Haiwezekani mchezaji kucheza vizuri kama hufanyi mapenzi na mwenza wako. Sijawazua kufanya hilo, na kama wanafanya basi ni wachezaji wazuri,” alisema Guardiola.
Tangu kuwasili kwa kocha huyo aliyewahi kuzifundisha Barcelona na Bayern Munich amefanya mabadiliko mbalimbali katika ikiwepo kuondoa huduma ya intaneti katika baadhi ya maeneo ya uwanja wa mazoezi wa klabu hiyo.
0 Maoni:
Post a Comment