PLUIJM ASAINI MIAKA MIWILI YANGA
YANGA imefanikiwa kumaliza utata wa kuendelea na kocha wao mkuu Hans Pluijm baada ya kumuongezea mkataba wa miaka miwili.
Mkataba wa Pluijm na Yanga ulifikia tamati mwezi mmoja uliopita ambao
ndiyo umeipa klabu hiyo mafanikio ya kutwaa taji la ubingwa wa VPL mara
mbili, Kombe la FA pamoja na kutinga hatua ya makundi Kombe la
Shirikisho.
Pluijm amesema anafuraha ya kuendelea kuifundisha Yanga ambapo sasa
anataka kuhakikisha anaendeleza kazi na mafanikio zaidi kwa Yanga kuweza
kufika mbali katika mashindano ya CAF mwakani.
“Naipenda hii klabu sikuzote nimekuwa nikifanya kazi kwa kutanguliza
heshima na mapenzi ambayo watu wa Yanga wamekuwa wakinionyesha, sasa
nimeongeza mkataba ambao hata familia yangu ina furaha na hilo,” amesema
Pluijm.
“Changamoto yangu kubwa sasa ni kuhakikisha Yanga inafanya mazuri
zaidi kuzidi ya haya tuliyoyapata msimu huu naju haitakuwa kazi rahisi
lakini hakuna namna lazima tupambane kila mmoja na nafasi yake kuweza
kufikia malengo.”
Mkataba huo wa Pluijm ambaye wikiendi iliyopita aliibuka kuwa kocha
bora wa msimu uliopita ameusaini mbele ya katibu mkuu wa Yanga Baraka
Deusdedit.
Ahsante kwa kutembelea site yangu, unaweza kunicheki kwenye mitandao ya kijamii kwa kubonyeza icons juu kulia na kunipata moja kwa moja kwenye Facebook, Twitter na Instagram...Endelea kuwa karibu yangu ili uweze kufikiwa na chochote kinachonifika.
0 Maoni:
Post a Comment