POLISI mkoani Dar es Salaam wamekamata mafurushi ya mifuko yakiwa na viungo mbalimbali vya binadamu vilivyohifadhiwa katika mifuko ya plastiki katika machimbo ya kokoto ya Bunju


POLISI mkoani Dar es Salaam wamekamata mafurushi ya mifuko yakiwa na viungo mbalimbali vya binadamu vilivyohifadhiwa katika mifuko ya plastiki katika machimbo ya kokoto ya Bunju wilayani Kinondoni, FikraPevu imefahamishwa.
Tukio hilo lililoibua hisia kali kwa wananchi limesababisha polisi kufyatua mabomu ya machozi kudhibiti wananchi waliofurika na kutaka kuvamia kituo cha polisi kumkamata dereva wa gari lililokutwa na viungo hivyo.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kipolisi wa Kinondoni, Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Cammillius Wambura ameithibitishia FikraPevu kukamatwa kwa viungo hivyo lakini hakuingia undani kutokana na kuwapo eneo la tukio Bunge, nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam, katika barabara iendayo Bagamoyo. 


Taarifa zilizoifikia FikraPevu usiku wa Jumatatu Julai 21, 2014 na kuthibitishwa Kamanda Wambura, zimeeleza kwamba viungo hivyo vimeokotwa katika machimbo hayo Jumatatu jioni vikiwa katika gari aina ya Toyota Hilux Pickup ikidaiwa kuwa ilifika hapo kwa mara ya pili kumwaga viungo hivyo.



"Ni kweli tumepata taarifa hizo muda mfupi uliopita na sisi tumefika katika eneo la tukio kwa taarifa zaidi tutawapa baadae tuko katika eneo la tukio hatuwezi tuzungumza," anasema Wambura. 

Taarifa zinasema miili hiyo imeonekana ikiwa imetelekezwa katika eneo hilo pamoja na kufungwa kwenye mifuko hiyo, ikiwa imekaushwa huku baadhi ya viungo vikionekana kua vya watu wazima. Mashuhuda wa tukio hilo wameiambia FikraPevu kuwa baada ya Jeshi la polisi kufika katika eneo la tukio wameondoka na miili hiyo kwa ajili ya uchunguzi zaidi.

Gari lakamatwa likiwa na shehena ya viungo vya binadamu
Katika tukio hilo polisi walitumia mabomu ya machozi na kupiga risasi za moto hewani, kutawanya wananchi waliovamia Kituo cha polisi cha Bunju 'A' wakitaka kumchukua na kumuua dareva aliyekamatwa na gari isiyofahamika namba mara moja ikiwa imesheheni viungo vya binadamu.

Taarifa zilizoifikia FikraPevu majira ya saa nne usiku zinadai kuwa, polisi katika Kituo cha polisi Bunju A na Wazo jijini Dar es Salaam, wamepiga mabomu ya machozi na risasi za moto hewani kwa lengo la kutawanya wananchi hao.

Mashuhuda wamesema kwamba wananchi walijawa na hasira baada ya kupata taarifa kwamba baadhi ya viungo vilikua havijakauka baadhi vikielezwa kuvuja damu.

Dereva huyo anadaiwa kummwaga viungo hivyo mara ya kwanza, katika Shule iliyotajwa kwa jina la Consolata inayomilikiwa na Kanisa Katoliki, na kuwa baada ya wananchi kushuhudia tukio hilo waliripoti polisi ambao waliofika na kulikamata gari hilo.
Share on Google Plus
Ahsante kwa kutembelea site yangu, unaweza kunicheki kwenye mitandao ya kijamii kwa kubonyeza icons juu kulia na kunipata moja kwa moja kwenye Facebook, Twitter na Instagram...Endelea kuwa karibu yangu ili uweze kufikiwa na chochote kinachonifika.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 Maoni:

Post a Comment