WABUNGE wa CHADEMA, Peter Lijualikali (Kilombero) na Suzan Kiwanga
(Mlimba) pamoja na washtakiwa wengine 37 ,jana wamefikishwa katika
Mahakama ya Hakimu Mkazi Morogoro kusikiliza maombi ya kupatiwa dhamana
kwenye kesi inayowakabiri.
Mahakama imetatoa uamuzi huo saa 9 alasiri leo baada ya mabishano ya
kisheria juu ya dhamana za Wabunge wa CHADEMA, Peter Lijualikali na
Suzan Kiwanga na washtakiwa wengine 36.
Itakuwambukwa kuwa, Washtakiwa hao kwa ujumla hao wanakabiliwa na
mashtaka manne likiwemo la kuchoma moto ofisi za serikali ya Kijiji cha
Sofi, wilayani Malinyi katika uchaguzi wa mdogo wa madiwani uliomalizika
hivi karibuni mkoani Morogoro.
Upande wa mastaka ukiongozwa na Sunday Hyera na Edga Bantulaki
uliwasilisha maombi mahakamani hapo kupingwa watuhumiwa kuachiwa kwa
dhamana kwa kile kilichoelezwa kuwa upelelezi wa kesi hiyo utaharibika.
Upande wa utetezi ukiongozwa na wakili Peter Kibatala ulipinga mamobi
hayo na kueleza kuwa kiapo hicho cha kupinga dhamana kilikuwa na
mapungufu mengi ya kisheria pamoja na kukosekana kwa uthibitisho wa mtu
aliyeandika kiapo hicho.
Baada ya pande zote mbili kuvutana kwa hoja za kisheria kwa takribani
saa 2, hakimu Ivan Msack aliahirisha kesi hiyo kwa muda na baadaye ndipo
ikaamuriwa waachiwe kwa dhamana.
0 Maoni:
Post a Comment