JPM kuzindua kampeni ya uzalendo leo

Rais John Magufuli
KAMPENI ya Kurudisha Uzalendo uliopotea miongoni mwa Watanzania itazinduliwa leo na Rais John Magufuli.
Akizungumza na vyombo vya habari mjini hapa jana, Waziri wa Habari, Utamaduni,Sanaa naMichezo, Dk Harrison Mwakyembe alisema uzinduzi wa kampeni hiyo utafanyika Ukumbi wa Chimwaga katika Chuo Kikuu cha Dodoma.
Alisema uzinduzi wa kampeni ya utamaduni na utaifa inalenga kurudisha uzalendo kutokana na kuwapo kwa dalili ya baadhi ya Watanzania kukosa uzalendo.
 Wakati huo huo, Rais John Magufuli amewasili mkoani Dodoma jana tayari kwa shughuli za uzinduzi wa kampeni hiyo pamoja na kushiriki sherehe za maadhimisho ya miaka 56 ya Uhuru zitakazofanyika katika Uwanja wa Jamhuri Mjini Dodoma kesho. 
Katika Ikulu ya Chamwino, Rais Magufuli amepokelewa na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Dk Binilith Mahenge.
Share on Google Plus
Ahsante kwa kutembelea site yangu, unaweza kunicheki kwenye mitandao ya kijamii kwa kubonyeza icons juu kulia na kunipata moja kwa moja kwenye Facebook, Twitter na Instagram...Endelea kuwa karibu yangu ili uweze kufikiwa na chochote kinachonifika.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 Maoni:

Post a Comment