SIMBA KUSHEREHEKEA USHINDI KATAVI

Related image
Simba SC jana imerudi kileleni mwa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara baada ya ushindi wa 1-0 dhidi ya Mbeya City 

KIKOSI cha Simba kimeondoka leo asubuhi mjini Mbeya kwenda Katavi mkoani Rukwa kwa ajili ya mchezo wa kirafiki dhidi ya wenyeji wao.

Mratibu wa Simba SC, Abbas Suleiman amesema leo kwamba wanakwenda Katavi kwa mchezo mmoja wa kirafiki utakaochezwa kesho na Jumatano watarejea Mbeya.

Simba SC ambayo jana ilirudi kileleni mwa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara baada ya ushindi wa 1-0 dhidi ya Mbeya City Uwanja wa Sokoine mjini Mbeya, itakuwa na mchezo mwingine wa Ligi Kuu mkoani hapa dhidi ya Tanzania Prisons Novemba 18. 

Mchezo huo uko mbali kwa sababu umepisha kalenda ya mechi za Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA), zikiwemo za kirafiki na kufuzu Kombe la Dunia. Wachezaji kadhaa wa Simba wanatarajiwa kuondoka kwenda kujiunga na timu zao za taifa na watakaobaki ndio watakwenda Katavi. 

Na Abbas amesema baada ya mchezo wa kesho kikosi kitarejea Mbeya kuendelea na kambi ya maandalizi, ila ukitokea mchezo mwingine wa kirafiki na benchi la Ufundi likauafiki watakwenda kucheza. 

Katika mchezo wa jana uliochezeshwa na refa Ahmed Kikumbo aliyesaidiwa na Omari Juma wote wa Dodoma na Michael Mkongwa kutoka Njombe, Simba ilipata bao hilo kipindi cha kwanza, likifungwa na winga, Shiza Ramadhani Kichuya. 

Kichuya alifunga bao hilo dakika ya saba baada ya mabeki wa Mbeya City kusita kumdhibiti wakidhani ameotea kufuatia pasi ndefu ya juu ya kiungo Jonas Mkude. 

Ushindi huo unaifanya Simba ifikishe pointi 19 baada ya kucheza mechi tisa na kupanda kileleni ikiizidi kwa wastani wa mabao tu Azam yenye pointi 19 pia. 

Share on Google Plus
Ahsante kwa kutembelea site yangu, unaweza kunicheki kwenye mitandao ya kijamii kwa kubonyeza icons juu kulia na kunipata moja kwa moja kwenye Facebook, Twitter na Instagram...Endelea kuwa karibu yangu ili uweze kufikiwa na chochote kinachonifika.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 Maoni:

Post a Comment