![]() |
MACHAKU |
Awali,
uongozi wa Lipuli uliwasimamisha wachezaji Malimi Busungu na Machaku
kutokana na utovu wa nidhamu waliokuwa wakiuonyesha katika klabu hiyo.
Akizungumzia suala hilo; Matola amesema kuwa, katika ripoti yake aliyoiwasilisha kwa uongozi, kuna majina kadhaa ya wachezaji ambao amependekeza kuachana nao akiwemo Machaku.
“Nimewasilisha
jina la Machaku kwa uongozi kuweza kuachana naye, simtaki aendelee
katika timu kwa kuwa ni mtovu wa nidhamu na hastahili kuwepo kwenye
timu.
“Awali
alikuwa yeye na Busungu, lakini mwenzie ameonekana kujirekebisha hivyo
nimeamua kumuacha aendelee, lakini kwa upande wa Machaku hana nafasi
tena ya kuendelea katika kikosi chetu.
“Nadhani
akiendelea kukaa katika timu atawaharibu wachezaji wengine kwani
nidhamu yake ni mbovu, hivyo sihitaji kuendelea kubaki naye, kwa sasa
nipo katika mchakato wa kutafuta wachezaji wengine kwa lengo la
kuimarisha kikosi ambapo nimepanga kusajili wachezaji watano katika
usajili wa dirisha dogo,” alisema Matola.
0 Maoni:
Post a Comment