
Mshambuliaji wa Borussia Dortmund
Pierre-Emerick Aubameyang ametemwa katika kikosi cha timu hiyo kutokana
na maswala ya ukosefu wa nidhamu.
Aubameyang hatashirikishwa katika mechi dhidi ya VFB Stuttgart siku ya Ijumaa.
Dortmund ilitangaza kumsimamisha kwa muda mchezaji huyo ikijibu maswali ya mashabiki wake katika Twitter, lakini haikuelezea sababu ya hatua hiyo.
Raia huyo wa Gabon pia alisimamishwa kwa muda mwaka uliopita baada ya kuelekea Italy bila rukhusa ya klabu hiyo.
''Sielewi ni kwa nini, nilizuiwa kuelekea Milan kwa sababu sikuheshimu sheria , lakini wakati huu nimekasirishwa sana , sikutaka kuwasili nikiwa nimechelewa'', aliambia gazeti la Bild nchini Ujerumani.
Dortmund imepoteza pointi tatu katika mechi zake nne na hivyobasi kushuka katika jedwali la ligi pointi sita
0 Maoni:
Post a Comment