
Mshambuliaji wa Arsenal Alexis
Sanchez hajamwambia mkufunzi wa Arsenal Arsene Wenger kwamba anataka
kuondoka katika klabu hiyo , kulingana na mkufunzi huyo ambaye
anatarajia mchezaji huyo wa Chile kukamilisha kandarasi yake.
Hatahivyo imeripotiwa kwamba Sanchez angependa kujiunga na wapinzani wa Arsenal Manchester City .
Alipoulizwa iwapo Sanchez alimwambia kwamba angependelea kuondoka , rais huyo wa Ufaransa amesema kuwa hapana.
Wenger aliongezea: Wachezaji wana kandarasi na tunawatarajia kuheshimu kandarasi zao , hilo ndio tunalotaka.
Sanchez alijiunga na Arsenal kutoka Barcelona kwa kitita cha pauni milioni 35, 2014.
0 Maoni:
Post a Comment