Katibu
wa Itikadi na Uenezi wa CCM Taifa, Humphrey Polepole amesema anayo
orodha ndefu ya viongozi wa upinzani wanaotaka kuhamia CCM.
Polepole
alisema hayo jana huku akibainisha kuwa orodha hiyo inahusisha
wenyeviti, madiwani na wabunge lakini siku nyingi tu alikuwa
amewakatalia kuwapokea.
Hata hivyo Polepole alisema kwamba kutokana na kutuhumiwa kuwanunua sasa anafanya kweli, atawachukua mmoja mmoja.
Polepole
alisema amemua kuchukua uamuzi huo baada ya Chadema kuonyesha utovu wa
nidhamu kwa kudai kuwa madiwani wanaokihama chama hicho wamehongwa na
CCM.
“Sasa tutaanza kumchomoa mmoja baada ya mwingine na kwa kutekeleza hilo wiki hii watampokea kiongozi mkubwa wa chama hicho,’’anasema Polepole.
Alibainisha kuwa kama chama kinakuwa na viongozi wanaoweza kuhongwa na wakahongeka basi chama hicho kitakuwa ni cha hovyo
"Madiwani
wamesema wanamuunga mkono John Magufuli, wametoka wenyewe wameanza
kusema CCM imewanunua, sasa kwa vile wameanza utovu wa nidhamu nitaanza
kumtoa mmoja baada ya mwingine,’’anasema.
Polepople anaongeza kwamba: “Nilikua
nakataa kuwapokea ila nina orodha kubwa wapo wenyeviti, wabunge kibao
kama vile watu wanaojisaliji kodi ya majengo TRA"
"Unajua
wanasema wanaisoma namba, nawahakikishia baada ya miaka mitano kwa
spidi hii iliyoanza nayo CCM namba inayoonekana wakati huu itakuwa
haisomeki kabisa, nitafanya shoo ndogo tu kuwachomoa viongozi hao
sipendi kwenda kuwachukua wengi sababu nitaonekana kama nawahujumu vile
na pia ili upinzani usikose watu angalau wa kuzungumza nao,"alisema
0 Maoni:
Post a Comment