BONDIA
Floyd Mayweather usiku wa jana alimwagia noti za dola za Kimarekani
mpinzani wake, Conor McGregor katika mwendelezo wa promosheni ya pambano
lao Agosti 26, mwaka huu.
Katika
mkutano huo wa tatu kuwakutanisha uso kwa uso kwa ajili ya ziara ya
promo la pambano lao, Mayweather alimuita McGregor muachaji akimanisha
hawezi kuvumilia kumalizia jambo na kisha akamrushia noti za dola
akisema; "Naendesha shoo, hi ni** yangu na na ninamwagia dola moja
huyu****."
Baada
ya siku tatu za promosheni, baadhi wamesema wawili hao wanakwenda nje
ya mstari, wakati pia wawili hao wameshindwa kuheshimiana.

Bondia Floyd Mayweather akijivuta pembeni baada ya kumwagia dola mpinzani wake, Conor McGregor usiku wa jana
Wakati wawili hao waliibuka watulivu safari hii, hakukuwa na msisimko hadi Mayweather aliposogea jukwaani na 'kulianzisha'.
McGregor
alimkandia Mayweather "uso kwa uso" mwanzoni kwa kumuambia anaelekea
kufilisika kama rafiki yake '50 Cent'. "Amefilisika na wewe unaelekea.'
Nyota huyo wa Ireland kisha akampa Mayweather albamu mpya ya Jay Z na kumuambia ampe 50 na amuambie 'blanco amekutumia'.
"Hawajui
mimi ni nusu mweusi? Mimi ni nusu mweusi haswa," alisema ili kujikosha
na tuhuma za ubaguzi wa rangi alizokwishaanza kutupiwa na kwenda kucheza
na shabiki wake wa kike mweusi.
Baadaye Mayweather akakamata kipaza sauti tena na kusema: "Unajua nini, ninakuka? ninanuka****'.
Kisha
akaugeukia umati kuuambia umnyooshee kidole 'muachaji' kabla mistari ya
wimbo 'Baby Tap Out' haijaanza kusikika kwenye spika kubwa.
Mbabe
huyo mwenye umri wa miaka 40 kisha akaanza kumtupia noti za dola
McGregor ambaye alijibu kwa mshituko: "Zote ni dola moja moja! Ziko wapi
fedha halisi?'
"Kwa sababu huo ndiyo utajiri wako wote," Mayweather akakasirika.
Mmarekani
huyo kisha akaonekana kutaka kumvaa mpinzani wake, kabla ya timu yake
kumuondoa McGregor. Timu ya bondia wa Ireland inayowahusisha Dillon
Danis na Owen Roddy, nayo haraka ikaingia, huku umati wa 19,000
uliokuwepo ukumbini ukishangilia.
Upinzani wao utaendelea Uwanja wa Wembley mjini London, Ijumaa jioni.
0 Maoni:
Post a Comment