Sadio Mane anatarajia kuanza mazoezi kamili wiki ijayo baada ya kupona majeraha ya goti na atashiriki mechi za kujianda.
Mane hajasafiri na timu kuelekea Asia kwa ajili ya mechi za kirafiki
kwa sababu anaendelea na matibabu yake lakini anatarajiwa kuwa fiti na
kujiunga na timu kwa ajili ya safari ya Ujerumani kukabiliana na Hertha
Berlin July 29.
Mane alifanyiwa upasuaji wa goti April baada ya kuumia katika mechi
ya ushindi wa 3-1 dhidi ya majirani zao Everton uwanjani Anfield.
“Sadio anaelekea kurudi ,”Alisema kocha Jurgen Klopp,”Plani atakwenda na sisi Ujerumani”.
“Tumekuwa tukisubiri kwa muda mrefu sasa.Yupo Melwood kila muda na afya njema”.
“Bahati mbaya hakuwa tayari kufanya mazoezi lakini anaonekana yuko vizuri,jeraha linaonekana kupona na atakuwa salama tukirudi”.
Mane alifunga magoli 13 msimu uliopita ya ligi baada ya kujiunga na Liverpool kwa ada ya £34m akitokea Southampton.
0 Maoni:
Post a Comment